Blogi (Blog) ni nini?/What is a blog?
Blogi ni tovuti ya habari ambayo taarifa zake huandaliwa
kila mara na kuwekwa kwenye www ambayo huwa na habari zilizogawanyika ktk
muundo wa vitokanavyo (post) ambazo huonekana kwa mfumo wa ya habari ya mwisho
kuingia ndiyo ya kwanza kusomeka mtu anapotembelea ukurasa mkuu katika tovuti
husika.
Namna ya kufungua blogi/How to open a Blog
Katika habari hii nataka kukuonesha namna nyepesi ya
kufungua na kuendesha blogi yako mwenyewe na kama hujawahi au hujui leo lazima
ujue tu usipoteze pesa wala muda wako kumuomba mtu kukufungulia blogi kwa ajili
yako.
Kama huna Gmail akaunti fungua kwa kufuata maelekezo hapa,
kama unayo fuatana na mimi.
Ukishakuwa na akaunti hiyo hakikisha umeingia katika akaunti
yako (sign in).
1. Baada ya hapo angalia kona ya kulia kama unatumia simu au
ngamizi/kompyuta (computer) utaona alama za vi boksi kama unatumia ngamizi.
Bofya sehemu iliyo andikwa moja kisha namba mbili kama ilivyo katika picha.
2. Chagua blogger kwa kobofya kitufe kilichoandikwa namba tatu.
3. Utapelekwa ukurasa mwingine kisha changua create new blog
halafu jaza nafasi zilizo andikwa nne na tano.
Namba nne ni kichwa cha blogi yako ambacho kitakuwa
kinaonekana juu katika ukurasa mkuu wa blogi yako. Namba tano ni jina la
kipekee ambalo halitakiwi kufanana na la blogi nyingine yoyote, kama ikitokea
basi utaambiwa halipo hilo jina jaribu kubadilisha jina. Na ningependekeza liwe
ni jina la kuelezeka au kuelezea blogi yako, lisiwe refu sana.
4. Baada ya kulipata jina hilo chagua mfano wa untakao uwe muonekano
wa blogi yako kutoka mojawapo ya mifano katika namba sita.
5. Mwisho bofya namba saba (create) subiri kidogo. Hongera umemaliza
kutengeneza



0 comments:
Post a Comment