ULIKUJA KUFANYA NINI HAPA DUNIANI?
Ni kitabu ambacho kiko katika lugha yetu pendwa ya Kiswahili, kinachojaribu kujibu pamoja na swali la kwa nini ulikuja hapa duniani, maswali kama nini maana ya maisha na furaha katika maisha. Kimesheheni falsafa za kweli zitakazokuwezesha wewe kuishi maisha ya furaha, yaana kujua na kufanya kile kilichokuleta hapa duniani.
Kimeandikwa na mwl. Kashindi Edison
Kashindi Edson ni nani?
Huyu ni Mwalimu na Mwandishi wa kitanzania, mbobezi katika elimu ya maisha ya binadamu, mtafiti wa masuala ya mafanikio, Saikolojia ya maisha na Falsafa za kweli kuhusu mafanikio na furaha ya kudumu katika maisha. Kashindi Edson anaamini kwamba kila binadamu aliyeko hapa chini ya jua kuna shughuli au kazi fulani ambayo alikuja kufanya hapa duniani. Na maisha ya kweli, furaha ya kweli huanzia pale tu unapotambua kile kilichompelekea MUUMBA wako kukuumba wewe na kukuleta hapa duniani na kuendelea kukuweka hai mpaka siku ya leo. "Ulikuja Kufanya Nini Hapa Duniani?" ni kitabu kinachoenda kukuambia wewe ni nani, una nini ndani yako na kukusaidia kujua kitu gani hasa ulikuja kufanya hapa duniani. Maisha hayana maana. Kinacholeta maana ni kile unachokifanya kila iitwapo leo katika maisha yako binafsi na katika maisha ya wengine. Chenye maana ni kusudi, sababu ya wewe kuwepo hapa duniani. Tafuta maana ya maisha, kutana na zungumza na Kashindi Edson ndani ya "Ulikuja Kufanya Nini Hapa Duniani?", kitabu kinachoenda kukupa fursa ya kusoma na kujifunza juu ya maisha yako ya sasa na kukuwezesha kuandika maisha yako mengine mapya unayoyatamani na kuyapenda kutoka nafsini mwako. Kufanya kile ulichokuja kufanya hapa duniani ndiyo kuishi maisha halisi, yenye amani iliyo ya kweli na si vinginevyo. Kufanya kile unachokipenda kutoka moyoni mwako ndiyo maana ya kweli ya maisha ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuishi. Kitabu hiki ni mwongozo wa kweli kuelekea maisha ya kweli. Karibu tuwe sote kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa mwisho kwa uvumilivu, umakini na utulivu. Huendi kusoma kitabu ila kitabu kinaenda kukusoma wewe.
Asante sana usisahau
Kujipatia Nakala ya kitabu chako, sasa kwa shilingi elfu 10/=
Wenzako wanaendelea kujipatia kitabu hiki na wanaendelea kuelimika....




0 comments:
Post a Comment