Kwanza tujifunze kidogo kuhusu ari watu waliyonayo juu ya mitandao ya kijami na jinsi inavokuza mawasiliano miongoni mwa jamii hasa jamii ya kimtandao, ambayo hutegemea sana huduma za kitovuti/ki elekroniki.
Watu wengi hutumia mitandao ya kijamii kupashana habari kwa haraka kwa hiyo ukitaka kuwafikia watu wengi kwa haraka jitahidi kutumia mitandao ya kijamii. Kama vile Jamii Forum, Facebook, twitter, whatsapp, linkedIn, Instagram, n.k.
Kwa sasa hakuna mtu ataweza kupinga kuwa whatsapp ndiyo mtandao rahisi kutumia na maarufu kwa wapashana habari.
Ikiwa unamiliki blogi au tovuti (website) na huna namna ya kuwapasha habari kwa haraka wafuasi wako kwa kubaki kutegemea wao wazitafute kwa wakati wao utabaki nyuma siku zote na wajanja na wafanya biashara wakubwa wameshtuka na kwa sasa huwasogezea huduma hizo viganjani mwao.
Aidha huzifanya habari na taarifa zao kuonekana kila mahali na kila wakati na zikiwa bado taarifa ni za moto kabisa. Kulijua hili, kwa sasa karibu kila mtandao wa kijamii uko na namna unavyoweza kuwasambazia wafuasi habari kutoka katika blogi, au tovuti mbalimbali kwa kutumia uwezo wa kusambaza (share).
NAMNA YA KUWEKA KISAMBAZIO (share button) CHA WHATSAPP
Kwanza uwe na blog yako ya blogger.com kama huna fuata maelekezo haya hapa namna ya kuifungua kirahisi na kwa njia ya kiswahili kabisa.
Nakuhakikishia ukiiweka iwe katika blogi au tovuti yako utafurahi sana na hutakaa usahau na utanikumbuka sana utapata watembeleaji mpaka ushangae
Kwanza kabisa nenda katika dashibodi ya blogi yako, bofya Theme, hafu Edit Template, kamata kitufe cha CTRL+F kisha katika kiboksi cha kuandika andika share na umalizie na kubofya ENTER kisha utamalizia kwa kuiweka sehem ya mwisho kama inavyoonekana katika picha hapa chini.
Ili uweze kufanikiwa tafadhali timia computer yako nenda. https://compcenta.blogspot.com




0 comments:
Post a Comment